Home BUSINESS NAIBU WAZIRI Dkt. KIRUSWA ATEMBELEA BANDA LA DIB MAONESHO YA MADINI GEITA

NAIBU WAZIRI Dkt. KIRUSWA ATEMBELEA BANDA LA DIB MAONESHO YA MADINI GEITA

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa (kushoto), akiwasili katika Banda la Bodi ya Bima ya Amana (DIB), nakupokelewa na  Mkurugenzi wa Bodi hiyo Bw. Isack Kihwili, (katikati), pamoja na Mhasibu Mwandamizi wa taasisi hiyo Bi. Kulwa James Kasuka (kulia), wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kutembelea Banda la taasisi hiyo, kwenye maonesho ya saba ya  teknolojia katika Sektsa ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja vya EPZ Bombambili Mkoani Geita.

DIB inashiriki maonesho hayo kwa mara ya kwanza kama taasisi inayojitegemea ili kujitangaza kwa wadau na wananchi, kufahamu majukumu yao wanayoyatekeleza kwa mujibu wa sheria.

Awali Taasisi hiyo ilikuwa ikitekeleza majukumu yake kama idara ndani ya Benki Kuu ya Tanzania BoT.

Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 2, nakufunguliwa rasmi tarehe 5, Octoba, 2024, na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko, yanatarajiwa kufungwa rasmi  Octoba 13, 2024 na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

(PICHA NA; HUGHES DUGILO)

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa (katikati) akisaini kitabu cha wageni mapema kabla ya kupata maelezo kuhusu majukumu ya taasisi hiyo. (kushoto), ni  Mkurugenzi wa Bodi hiyo Bw. Isack Kihwili, na (kulia), ni Mhasibu Mwandamizi  wa Bodi hiyo Bi. Kulwa James Kasuka

Mkurugenzi wa Bodi ya Amana – DIB- Bw. Isack Kihwili, (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa (katikati) alipokuwa katika Bamda la taasisi hiyo kufahamu kazi wanazozifanya. (kulia), ni Mhasibu Mwandamizi  wa taasisi hiyo Bi. Kulwa James Kasuka.

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa (kulia), akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Bodi hiyo Bw. Isack Kihwili, (kushoto)

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa (kushoto), akisalimiana na Afisa wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB) Careen Max (katikati), mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea Banda la taasisi hiyo. (kulia), ni Mhasibu Mwandamizi  wa DIB Bi. Kulwa James Kasu ka

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here