Home ENTERTAINMENTS MTIFUANO MKALI, USAHILI BONGO STAR SEARCH AFRIKA KUANZIA ARUSHA 

MTIFUANO MKALI, USAHILI BONGO STAR SEARCH AFRIKA KUANZIA ARUSHA 

USAHILI wa Wasanii wa Shindano la Bongo Star Search African kuanza kufanyika Mkoani Arusha Novemba 9 hadi 10 katika ukumbi wa SG Resourt Mianzini.

Akitaja maeneo ambayo usahili utafanyika wa Bongo Star Search African Mkurugenzi wa Benchmark Ritha Poulsen ‘Madam Ritha’ amesema kuwa Usaili utaanza Arusha na baadae Mkoani Mwanza.

“Mkoani Arusha Novemba 9 hadi 10 2024 SG Resourt Mianzini, Mwanza Novemba 16 hadi 17 mwaka huu La Kairo Hotel, Kampala Novemba 23 hadi 24 mwaka huu, Nairobi Novemba 30 hadi 01DEC 2024 Little Thiether Babati Desemba 6 hadi 7 Olympic Lounge huku Dar es Salaam ikiwa Decemba 13 hadi 15, 2024 katika ukumbi wa Makumbusho ya ya Taifa Bongo Star Search Afrika!

Madam Ritha aliongeza kwa kuwashukuru wadhamini kwa kuendelea kuwashika mkono kwa juhudi wanazofanya kuendeleza tasnia ya burudani nchini.

“Kwa wadhamini wetu na washirika wa Bongo Star Search, tunatoa shukrani,
hamjawa tu wadau, bali ni sehemu muhimu ya mafanikio ya mpango huu. Ushirikiano wenu umetufanya kufikia malengo haya ya kupanua wigo na kufikia zaidi ya mipaka ya Tanzania.”amesema Madam Ritha

Mashindano hayo yataonyeshwa kupitia vyombo mbali mbali vitakazo kuwa vinaonesha kipindi chetu moja kwa moja
Tanzania: St Swahili Channel ndani ya Star Times Uganda: Makula Tv Nairobi: St Swahili ch 160 & 400.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here