Aidha amekabidhi Mashine ya kudurufu yenye thamani ya Sh Milioni 3 ikiwa ni ahadi aliyoitoa mwaka jana 2023 kwenye mahafali kama hayo.
Akizungumza katika mahafali hayo Octoba 2,2024,Mtaturu amewahimiza Wazazi kuendelea kushirikiana na Walimu kwenye kuwasimamia Wanafunzi kwenye taaluma na maadili.
“Nimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha nyingi za maendeleo kwenye jimbo la Singida Mashariki,wananchi wenzangu haya ninayoyasema yanaonekana kwa macho,miradi inatekelezwa kwa vitendo,”.amesema.
Mtaturu ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kuendelea kujiandikisha kwenye daftari la mkaazi litakaloanza tarehe 11 hadi 20 Octoba 2024 ili wapate sifa ya kupiga kura tarehe 27 Novemba 2024 kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa Serikali za mitaa, Vijiji na Vitongoji.
Akisoma risala Mkuu wa shule hiyo ameeleza mafanikio waliyoyapata ikiwemo kuongeza ufaulu kutoka asilimia 77 mwaka 2022 hadi asilimia 82 mwaka 2023.
Aidha amesema kama shule wamepokea Sh Milioni 42 kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo ya kisasa ya walimu na wanafunzi na Sh Milioni 55 kwa ajili ya kujenga shule bora ya Chekechea pamoja na vyumba vya madarasa.
“Tunakushukuru Mbunge wetu kwa kuendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia hapa shuleni,jitihada zako tunaziona,”amesema.
Diwani wa Kata ya Ikungi Abely Nkuwi amempongeza Mbunge Mtaturu kwa kuwa sauti ya Wana Singida Mashariki na maendeleo yanaonekana kila mahali na kusema watamlipa kura za kishindo pamoja na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan 2025.
#SingidaMashariki#MaendeleoHayazuiliki#ManenoKidogoKaziKidogo#