Home LOCAL MIFUMO YA TAASISI 7 IMEANZA KUSOMANA

MIFUMO YA TAASISI 7 IMEANZA KUSOMANA

Katika mwaka 2023/24, Kituo cha Uwekezaji kimekamilisha ujenzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Kuhudumia Wawekezaji (Tanzania Electronic Investment Window – TeIW) kwa awamu ya kwanza ambao ulizinduliwa Septemba, 2023

Mfumo huo umeunganishwa na mifumo ya Taasisi saba (7) ambazo ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji, Idara ya Kazi, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na TIC.

Mfumo huo, unamuwezesha mwekezaji kusajili mradi popote ndani na nje ya nchi na kupata vibali vya uwekezaji ndani ya siku 3 ikiwa ametimiza vigezo.

Awamu ya pili ya ujenzi wa mfumo huo itahusisha uunganishaji wa Taasisi nyingine saba (7) ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Wizara ya Kilimo, Tume ya Madini na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here