Home LOCAL MCHUNGAJI TENGWA: WATANZANIA WANA KILA SABABU KUDUMISHA AMANI KIPINDI CHA UCHAGUZI

MCHUNGAJI TENGWA: WATANZANIA WANA KILA SABABU KUDUMISHA AMANI KIPINDI CHA UCHAGUZI

MCHUNGAJI wa Kanisa la Uamsho na Matengenezo ya Kiroho Ulimwenguni, Mwalimu Augustine Tengwa amewashauri watanzani katika kuelekea uchaguzi wa mwaka 2024, 25 kuhakikisha wana jukumu la kulinda Amani ya nchi na kuwakemea pia kuwakataa watu au wanasiasa wachochezi.

Ameyasema hayo leo Oktoba 11,2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameangazia umuhimu wa maombi ya kuliombea Taifakuelekea uchaguzi.

Mchungaji Tengwa akiwa ameambatana na wachungaji wasaidizi katika huduma hiyo yenye makao makuu mkoani
Morogoro amesema, kupitia maombi ambayo wamekuwa wakiyafanya mfululizo, Mungu amewaonesha ishara ambayosi njema katika chaguzi zijazo nchini.

Aidha amevishauri vyombo vya ulinzi na usalama kusimama vema katika nafasi zao ili kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika zaidi kabla na baada ya chaguzi zijazo.

Amesema, kutokana na hali hiyo kila Manzania analo jukumu la kuhakikisha amani ya nchi inatawala na wanapaswa kuwakemea ikiwemo kuwakataa watu wanasiasa wachochezi.

Tengwa ameongeza kuwa , Tanzania ni ya Watanzania na hawana taifa mbadala la kukimbilia iwapo wataruhusu wenye nia ovu kutimiza matakwa yao ili kupata nafasi za uongozi.

Kwa upande wake, Nabii Alpha Kiamba amewataka Watanzania kuyapa kisogo maneno na taarifa zenye viashiria vya kuwagawa ambavyo vimekuwa vikizushwa na baadhi ya wanasiasa wakiwemo wanaharakati mbalimbali.

“Na, suala la upinzani nchini lifanyike katika hekima za Mungu, kwani taarifa zinatolewa ili kuliokoa Taifa na mauti.

“Ndiyo maana tutahitaji watu waombe, kila mkoa watu waingie kwenye maombi.Sasa Mama naye mnampiga mawe usiku na mchana” amesema

Amesema, mara nyingi wamekuwa wakifanya maombi na wanaamini Tanzania bila maombi hakuna taifa.

“Tumekuwa na kasumba fulani ya kupuuza taarifa kwa kuwa eti inatoka Mbinguni…ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here