Home BUSINESS MBIBO AZUNGUMZA NA UJUMBE KUTOKA RUSSIA

MBIBO AZUNGUMZA NA UJUMBE KUTOKA RUSSIA

*GST kushirikiana na Federal Agency For Minerals Resources of the Russian Federation Utafiti wa Madini*

Dar es salaam,

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo ametoa wito kwa Wawekezaji kuchangamkia fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini ikiwemo kuwekeza kwenye kufanya tafiti za Jiolojia kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa ili kuvumbua maeneo mapya ya uchimbaji madini.

Mbibo amesema hayo leo Oktoba 29, 2024 alipokutana na kuzungumza na ujumbe kutoka Federal Agency for Minerals Resources of Russian Federation Jijini Dar es salaaam uliyokuwa ukishiriki Mkutano wa Tanzania-Russiaan Business and Investment Forum.

Katika Mazungumzo hayo, Mbibo amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Federal Agency for Minerals Resources of the Russian Federation na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili kuleta tija katika tafiti za pamoja.

Katika hatua nyingine, Mbibo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Uendelezaji Biashara akiwakilisha Sberbank International katika Ukanda wa Subsaharan Afrika ili kuangalia uwezekano wa kushiriki katika kufadhili miradi ya Utafiti na uchunguzi wa majanga ya Jiolojia ikiwemo Matetemeko ya ardhi, kububujika kwa tope, mafuliko nk.

Aidha, Mbibo ameeleza kuwa, Tanzania ni nchi salama kwa uwekezaji na kuusisitiza ujumbe huo kuwekeza kwenye kufanya Utafiti wa Jiolojia kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa ili kubaini maeneo mapya yenye viashiria vya madini.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Federal Agency For Minerals Resources of the Russian Federation, Andrey Vorobieve amemhakikishia Naibu Katibu Mkuu kwamba mambo yote waliyozungumza katika mazungumzo yao na yaliyozungumzwa kwenye Mkutano wa siku mbili yote yatatekelezeka kupitia mashirikiano.

Sambamba na hapo, Mkutano huo ulitanguliwa na kikao cha wataalamu kilichofanyika Oktoba 28, 2024 ambacho pia Naibu Katibu Mkuu alishiriki pamoja na Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here