Home BUSINESS MAMLAKA YA BANDARI YASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA MADINI GEITA

MAMLAKA YA BANDARI YASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA MADINI GEITA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA inashiriki katika Maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya Bomba mbili Mkoani Geita.

Mamia ya Wananchi wanaotembelea maonesho hayo wamevutiwa na Banda la TPA ambalo limesheheni vifaa vya mfano vinavyotumika kutolea huduma Bandarini ambavyo vimekuwa kivutio kikubwa.

Maonesho hayo yamefunguliwa tarehe 05 Oktoba 2024 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko. TPA ni miongoni mwa Wadhamini wa maonesho hayo.

       

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here