Home LOCAL KITUO CHA AFYA SUMBAWANGA  KUHUDUMIA WANANCHI ZAIDI YA HAMSINI

KITUO CHA AFYA SUMBAWANGA  KUHUDUMIA WANANCHI ZAIDI YA HAMSINI

Kituo cha Afya Sumbawanga Asilia kilichopo Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa kinatarajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya elfu hamsini na Kata za Jirani Momoka na Mafulala.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 2, 2024 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi Pindi Chana wakati akiweka jiwe la msingi katika kituo hicho.

Mhe. Chana amesema kituo hicho kimetumia takribani milioni 250 hivyo kitarahisisha upatikanaji wa huduma ya afya kitakapokamilika.

Amemuelekeza Mkandarasi anayejenga Kituo hicho kukikamilisha kazi kwa wakati ili wananchi wapate huduma bora.

Aidha, amewataka wananchi kukitunza na kukitumia vizuri kituo hicho kwa manufaa ya afya zao.

Naye, Kaimu Mganga Mkuu, Dkt. Louis Massawe amesema kwa sasa mradi uko katika hatua za mwisho za ukamilishaji ikiwemo uwekaji wa vigae pamoja na vioo.

Amesema mradi huo unajumuisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Maabara na Choo cha nje hadi kufikia sasa jumla ya shilingi milioni 163.8 zimeshatumika.

Previous articleIFIKAPO 2030 KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – BASHE
Next articleDKT NCHEMBA AISHUKURU IMF KWA KUCHANGIA MAENDELEO YA NCHI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here