Home BUSINESS EWURA YAZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUACHA KUPIKA TAKWIMU ZA HUDUMA

EWURA YAZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUACHA KUPIKA TAKWIMU ZA HUDUMA

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile (aliyesimama) akizungumza na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Wilaya na Mijimdogo. Kulia ni Mkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira, Mha. Exaudi Fatael Maro na kulia ni Mha. Jovitus Kichum kutoka Wizara ya Maji.
Na.Mwandishi Wetu-DODOMA
MAMLAKA za Maji na Usafi wa Mazingira nchini zimeelekezwa kutoa taarifa sahihi kuhusu uendeshaji na utoaji wa huduma kwa kuwa taarifa hizo hutumika katika utekelezaji wa mipango ya Serikali inayolenga kuimarisha sekta ya maji nchini.
Maelekezo hayo yametolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile, wakati akifungua kikao kazi cha kuhakiki taarifa kwa watendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira za Wilaya na Mijimidogo, jijini Dodoma.
Dkt. Andilile alisema kuwa, EWURA imetathmini taarifa zote zilizowasilishwa na Mamlaka hizo katika mfumo wa MajIs kwa Mwaka 2023/24 na kubaini takwimu zisizo sahihi za kiwango cha maji yanayozalishwa, muda wa upatikanaji wa huduma, usimamizi wa usafi wa mazingira,hali ya upatikanaji na kiwango cha uhitaji wa maji,ubora wa maji pamoja na upotevu wa maji.
“Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora ya maji na inayokidhi mahitaji yao ya kila siku, tunapokosa takwimu sahihi, ni ngumu kuwapatia wananchi huduma hiyo, hivyo mnatakiwa mtoe kipaumbele katika kuwasilisha takwimu na ziwe sahihi.
Kwa upande wake Mhandisi Jovitus Kichum, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, aliwasisitiza watendaji hao kuhakikisha takwimu zinazowekwa kwenye mfumo wa MajIs zinaakisi uhalisia ili Serikali iweze kutatua changamoto zinazojitokeza kwa lengo la kuimarisha huduma za majisafi na usafi wa mazingira nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile (aliyesimama) akizungumza na watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Wilaya na Mijimdogo. Kulia ni Mkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira, Mha. Exaudi Fatael Maro na kulia ni Mha. Jovitus Kichum kutoka Wizara ya Maji.
Watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Wilaya na Mijimidogo wakiendelea kuhakiki taarifa katika mfumo wa MajIs wakati wa kikao kazi kilochoratibiwa na EWURA, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt James Andillile (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Wilaya na Mijimidogo wakati wa kikao kazi cha kuhakiki taarifa za utendaji wao jijini Dodoma leo 30 Octoba 2024.Wengine ni Mkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira EWURA, Mha. Exaudi Fatael Maro ( kulia) na Mhandisi. Jovetus Kichum kutoka Wizara ya Maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here