Ofisa Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Getrude Mbiling’i (kulia) akimuelekeza mteja kujaza fomu ya malalamiko kuhusu huduma zinazodhibitiwa na EWURA katika viwanja vya Shule ya Msingi Uyui Tabora ikiwa ni sehemu ya maadhimishk ya Wiki ya Huduma kwa Mteja iliyoanza iliyoanza leo Oktoba 7,2024.
Watumishi wa EWURA Kanda ya Magharibi wakikata keki kuashiria kuanza kwa Wiki ya Huduma kwa Mteja, mjini Tabora leo Oktoba 7,2024.
Watumishi wa EWURA katika picha ya pamoja tayari kuwahudumia wananchi na wadau wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja, iliyoanza leo Oktoba 7,2024.
Na.Mwandishi Wetu.
MAMLAKAÂ ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi imepokea, kusikiliza na kutatua malalamiko ya wateja yanayotokana na huduma zinazodhibitiwa na EWURA katika sekta za nishati(umeme, mafuta, gesi asilia) na maji na usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja yaliyoanza leo 7/10/24.
Kaimu Meneja wa Kanda hiyo, Mha. John Kitonga amesema EWURA itatoa huduma hiyo kwa wateja kwa wiki nzima ( 7-11 Oktoba 2024) katika viwanja vya shule ya Msingi Uyui,manispaa ya Tabora ili kuwafikia wateja wenye uhitaji wa huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka.
“Wateja na wadau wetu,tembeeleni banda la EWURA hapa Uyui mpate huduma za moja kwa moja za utatuzi wa malalamiko, maombi ya leseni na vibali vya ujenzi,changamkieni fursa hii”. Alilisitiza.