Home LOCAL DUWASA YAPONGEZWA JITIHADA ZA HUDUMA YA MAJI DODOMA

DUWASA YAPONGEZWA JITIHADA ZA HUDUMA YA MAJI DODOMA


Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa jitihada inazochukua za muda mfupi za uchimbaji visima maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dodoma kuhakikisha wananchi waliyopo katika maeneo ya pembezoni wanapata huduma ya maji.

Pongezi hizo zimetolewa leo Oktoba 09, 2024 wakati wa Kikao cha Kamati ya PAC kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Naghenjwa Kaboyoka.

Aidha, Kamati hiyo imeiagiza DUWASA kufanyia kazi kwa wakati Hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).






LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here