Home LOCAL DKT. BITEKO ATAKA UMOJA, USHIRIKIANO NA UBUNIFU TAASISI ZA NISHATI

DKT. BITEKO ATAKA UMOJA, USHIRIKIANO NA UBUNIFU TAASISI ZA NISHATI

*Asema Rais Samia anataka Ubunifu ili kusogeza huduma bora kwa wananchi*

*Asisitiza utendaji kazi umuangalie Mtanzania wa kawaida anayeitegemea Serikali kubadili maisha*

*Ataka Watendaji waache alama ya kazi, si kulinda vyeo*

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watendaji na Watumishi katika Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati kuwa na umoja, ushirikiano na ubunifu ili kusogeza huduma bora kwa wananchi  ikiwemo za umeme, mafuta, Na Nishati Safi ya Kupikia.

Amesema hayo tarehe 28 Oktoba, 2024 jijini Dodoma wakati wa Kikao chake na Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake ambacho ni cha pili kutoka uanzishwe mfumo  mpya ndani ya Wizara na Taasisi zake wa kujifanyia tathmini ili kuona namna inavyofanya kazi ya kuhudumia wananchi.

Previous articleBANKI YA CRDB YATUNUKIWA TUZO ZA ‘BENKI BORA’ NA SALAMA TANZANIA NA JARIDA LA GROBAL FINANCE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here