Afisa kutoka Bodi ya Bima ya Amana (DIB) Careen Max (kulia), akizungumza na wadau kutoka Benki ya Azania waliotembelea katika Banda la Bodi hiyo kwenye maonesho ya saba ya Teknolojia katika Sekta ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya EPZ Bombambili mkoani Geita.
DIB inashiriki katika maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi kufahamu majukumu na kazi wanazofanya kwa mujibu wa sheria.