Home BUSINESS BoT YAWAKARIBISHA WACHIMBAJI KUUZA DHAHABU ZAO

BoT YAWAKARIBISHA WACHIMBAJI KUUZA DHAHABU ZAO

Mchambuzi wa  masuala ya fedha kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania ( BoT), Joshua Mganga (kushoto), akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Benki hiyo kwenye maonesho ya saba ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZ Bombambili Mkoani Geita.

Isa Pagali Meneja Msaidizi, Idara ya Uchumi  Benki Kuu Tawi la Mwanza  Isa Pagali (kushoto) akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea katika banda la BoT katika maonesho ya Madini Geita

Mchambuzi wa masuala ya kofedha Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za fedha  Charles Kanuda, (kushoto) akitoa elimu kuhusu huduma hizo katika maonesho ya Madini mjini Geita. 

Afisa mkaguzi Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha  Mamy Katikiro (kulia), akitoa elimu kwa wananchi waiofika kwenye banda la BoT ili kufahamu shughuli za benki hiyo. 

Na: Mwandishi wetu, GEITA 

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeweka mkazo kwenye umuhimu wa wachimbaji wa madini, hususan wachimbaji wadogo, kuuza dhahabu yao moja kwa moja kwa BoT ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa na kuimarisha thamani ya shilingi.

Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari  kwenye maonesho ya madini yanayoendelea mkoani Geita, Mchambuzi wa Masoko ya Fedha kutoka BoT Joshua Mganga,  amesema dhahabu ni rasilimali muhimu kwa uchumi wa Tanzania na kwa kuuzwa BoT, kutaongeza akiba ya fedha za kigeni na kuimarisha uthabiti wa shilingi dhidi ya sarafu za kigeni.

Aidha ameongeza kuwa uwepo wa akiba ya dhahanu BoT kutaiwezesha nchi kupata mikopo kwa urahisi kutoka taasisi za fedha za kimataifa.

“Mpango huu wa BoT kununua dhahanu kutawanufaisha moja kwa moja wachimbaji wetu  kwani utaratibu wa malipo ni wa haraka, unaofuata bei ya soko la Dunia  na kulipwa ndani ya saa 24.

“Sio tu kwamba wachimbaji wataweza kupata faida bali pia nchi itafaidika kwa kupata ongezeko la akiba ya dhahabu na kuepusha upungufu wa fedha za kigeni,” ameongeza.

Aidha, amemshukuru  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, kwa juhudi zake za kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali, wachimbaji, na masoko ya dhahabu ili kuhakikisha nchi inanufaika ipasavyo na rasilimali ya madini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here