Askofu Dkt. Frederick Shoo ameeleza kwa uzito kuwa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ni ishara thabiti kuwa wanawake wana uwezo sawa wa kuongoza, akimtaja kama mfano wa kimungu wa kuwatia moyo Watanzania. Alihimiza jamii kuachana na dhana potofu za kijinsia na kuwatazama wanawake kama viongozi waadilifu na wenye uwezo katika jamii na kanisa.
Aidha, Askofu Shoo ametoa kauli ambayo wengi huinong’ona lakini wachache huisema wazi—kwamba baadhi ya ukosoaji dhidi ya Rais Samia unatokana na jinsia yake, ikizingatiwa jamii yetu ya kihafidhina ambayo haijazoea kiongozi mwanamke.
Watanzania wanapaswa kutafakari maneno ya Warumi 13:1: “Kila mtu na atiye mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo imewekwa na Mungu.”Kwa mafanikio ya uongozi wake ndani ya muda mfupi, ni dhahiri kuwa Mungu yuko pamoja naye na anamtumia kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania