Home BUSINESS AJALI USAFIRI MAJINI ZAPUNGUA GEITA 

AJALI USAFIRI MAJINI ZAPUNGUA GEITA 

  

Geita.

Mkoa wa Geita umeripotiwa kutokuwa na ajali za majini katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/25 (Julai-Septemba 2024/25) ukilinganisha na vipindi vingine vilivyopita, hii ni kutokana na elimu inayoendelea kutolewa kwa wadau wanaotumia usafiri huu.

Akizungumza katika banda la Shirika Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Afisa Mfawidhi Bw. Godfrey Mtwena Chegere, katika mahojiano na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya saba ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZ Bombambili mkoani Geita.

“TASAC mkoa wa Geita inaendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kuchukua tahadhari na hii imepelekea kupungua ama kutokuwa na ajali hususan katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/25 amesema Bw. Chegere.

Aidha ameongeza kuwa ushiriki wa TASAC katika maonesho hayo ni kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi na majukumu yanayoyatekeleza kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415, na kwamba inawaalika wananchi wote kutembelea katika  banda lao.

“Tunaendelea kutoa elimu katika sehemu mbalimbali ikiwemo katika mialo, vivuko na hata kwenye maonesho kama haya ili kuhakikisha ajali zinaendelea kupungua siku hadi siku na kuhakikisha usalama wa wavuvi, wasafirishaji na wamiliki wa vyombo unakuwa Madhubuti,” ameongeza Chegere.

TASAC inashiriki katika Maonesho ya 7 ya Teknolojia na Madini yanayofanyika Mkoani Geita katika viwanja vya Bombambili. Maonesho hayo yameanza tarehe 02 Oktoba, 2024 na yanatarajiwa kufunguliwa siku ya Jumamosi tarehe 5 Oktoba, 2024 na Naibu Waziri Mkuu na Wazriri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko na kufungwa tarehe 13 Oktoba, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

      

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here