Home ENTERTAINMENTS WAZIRI NDUMBARO AMUONGEZEA FAINI SHILINGI MILIONI 5 BABU WA TIKTOK, ATOA WIKI...

WAZIRI NDUMBARO AMUONGEZEA FAINI SHILINGI MILIONI 5 BABU WA TIKTOK, ATOA WIKI MBILI ALIPE

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro
ameongeza adhabu ya faini kutoka shilingi milioni 3 hadi milioni 5 kwa msanii Seif Kisauji maarufu (Babu wa TikTok) akimtaka msanii huyo aombe msamaha hadharani kutokana na kosa la kurusha maudhui ya sanaa yanayokiuka maadili mtandaoni.

Waziri Ndumbaro ametoa uamuzi huo leo Septemba 3, 2024 Mtumba Jijini Dodoma baada ya kusikiliza rufaa ya msanii huyo ya kupinga adhabu aliyopewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ya kufungiwa kujihusisha na shughuli za sanaa kwa miezi 6 pamoja na kulipa faini ya shilingi milioni 3 kutokana na kurusha mtandaoni picha za video zinazokiuka maadili.

Aidha, kufuatia rufaa hiyo, msanii Seif Kisauji amekiri kosa la kusambaza maudhui hayo na kuomba apunguziwe adhabu hatua iliyomfanya Waziri Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro amuondolee adhabu ya kifungo cha cha miezi 6 cha kutojihusisha na shughuli za sanaa huku akimuongezea kiwango cha faini kutoka milioni 3 hadi 5.

Sheria ya BASATA iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 kifungu cha 15 A inampa mamlaka Mhe. Waziri kusikiliza rufaa na kutoa maamuzi, hivyo kwa kushauriana na Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma ambaye ndiye msimamizi wa sekta ya sanaa, nimefuta adhabu ya miezi sita aliyopewa kuanzia leo, na ninamtaka azingatie maadili katika kufanya kazi zake” amesisitiza Mhe. Ndumbaro.

Awali katika kikao hicho Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma alimataka Msanii huyo, kurudi katika sanaa aliyokua akiifanya zamani ambayo ndiyo iliyomfanya jamii imtambue na kuelewa kuwa yeye ni kioo cha jamii hivyo anapaswa kufanya Sanaa inayoelimisha na kuburushisha jamii bila kuharibu mila na desturi za Kitanzania.

Kwa upande wake Msanii Seif Kisauji ameishukuru wizara kukubali rufaa yake pamoja na kuridhia msamaha na kumfungulia kufanya sanaa akiahidi kujirekebisha na kufanya sanaa zenye maadili na kuwa Balozi mzuri kwa wasanii wenzake.

Previous articleRAIS SAMIA KUWA MWENYEKITI JUKWAA LA VIONGOZI WAKUU AFRIKA NA CHINA
Next articleMWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MHE.HAMZA JOHARI AMEWASILISHA MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO BUNGENI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here