Home BUSINESS WAZIRI MKUU ATOA MAELEKEZO UENDESHAJI MRADI WA SGR

WAZIRI MKUU ATOA MAELEKEZO UENDESHAJI MRADI WA SGR

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Uchukuzi iendelee kulisimamia kwa karibu Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kuhakikisha huduma za treni ya SGR zinaboreshwa na miundombinu inaimarishwa ili mradi huo uweze kudumu kwa muda mrefu.

Amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali itaendeleza sekta ya uchukuzi ambapo pamoja na mambo mengine itasimamia sekta ya reli ikiwemo ujenzi wa SGR na uendeshaji wa treni ya kisasa ya abiria kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa tarehe 31 Desemba, 2023 Mheshimwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alielekeza kuanza uendeshaji wa reli ya SGR kwa kipande cha Dar es Salaam – Dodoma ifikapo mwezi Julai, 2024.

Previous articleKIWANDA CHA MAFUTA YA ALIZETI KUNUFAISHA WAKULIMA DODOMA
Next articleNAIBU KATIBU CCM  AMEKUTANA NA WAJUMBE WA CCM SHINYANGA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here