Home BUSINESS WAZIRI BASHE ATEMBELEA SHAMBA LA KUZALISHA MBEGU ZA SHAIRI RUVUMA

WAZIRI BASHE ATEMBELEA SHAMBA LA KUZALISHA MBEGU ZA SHAIRI RUVUMA

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) ametembelea shamba la kuzalisha mbegu za shayiri la kampuni ya Silverland Ndolela Limited, tarehe 18 Septemba 2024 lililopo mkoani Ruvuma.

Amepitia mashine na Mifumo mbalimbali ya uzalishaji wa mbegu na kujadili namna ya kushirikiana nao, ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership – PPP), katika kujifunza na kubadilishana uzoefu wa matumizi ya teknolojia za kilimo na umwagiliaji kama vile matumizi ya mfumo wa “pivot system” na kilimo cha kisasa ili kuongeza tija katika uzalishaji.

Mbegu na mazao mengine yanayozalishwa na mengine kampuni hiyo ni pamoja na mahindi, maharage, ngano na alizeti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here