Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na kauli zinazotia mashaka kwa wananchi juu ya matukio ya kupotea kwa watu.
Watu wengi wamekuwa wakihusisha na kulituhumu jeshi la Polisi bila kufanya uchunguzi wa kina ikiwe Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekuwa kikitoa madai kuwa wanachama na wafuasi wake kadhaa wametekwa na serikali.
Hata hivyo, uchunguzi unaonesha kwamba madai haya yanakosa ukweli na yanatumika zaidi kama propaganda za kisiasa.
Uhalisia ni kwamba watu wengi ambao Chadema inadai wametekwa na serikali, kwa hakika ni watu wenye shughuli za kibiashara zinazotia shaka.
Mfano mzuri uliofanyika katika mkoa wa Rukwa ambao kupitia takwimu za TCRA mikoa inayoongoza kwa matukio ya simu za ulaghai hadi kufikia Desemba mwaka 2023 na idadi ya kwenye mabano ni Rukwa (7,666) na Morogoro (7,171), Dar es Salaam (1,717), Mbeya 1,549, Tabora 590 na Songwe 328.
Kuna uwezekano mkubwa kuwa ndugu Dioniz, ambaye Chadema wanadai ametekwa. Uchunguzi unaonesha kuwa Dioniz alikuwa anajihusisha na biashara zisizo halali, na kutekwa kwake kunahusishwa na biashara zake na wala jeshi la polisi halihusiki.
Ni muhimu kwa umma kuelewa kwamba serikali ina jukumu la kuhakikisha usalama wa raia na kushughulikia vitendo vyote vya uhalifu bila kujali itikadi za kisiasa za wahusika. Madai ya Chadema yanaonekana kuwa ni jaribio la kutumia hali hizi ili kuhalalisha ajenda zao za kisiasa na kujionyesha kama wahanga wa mateso ya kisiasa.
Serikali itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kulinda sheria na usalama wa nchi bila kubagua, na itachukua hatua stahiki dhidi ya yeyote anayejiingiza katika shughuli za kihalifu, bila kujali ni chama gani cha siasa anachotoka. Madai ya utekaji wa wanachama wa Chadema yanapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa, kwani yanaweza kuwa na nia ya kupotosha umma na kuendeleza ajenda za kisiasa zisizo na msingi.