Home LOCAL TEKELEZENI KWA VITENDO FALSAFA YA 4R YA RAIS DKT. SAMIA-MAJALIWA

TEKELEZENI KWA VITENDO FALSAFA YA 4R YA RAIS DKT. SAMIA-MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Maafisa waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na viongozi wa vyombo vya usalama wa Wizara hiyo kutekeleza kwa vitendo na kuiishi falsafa ya R nne (4R) ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Amesema kuwa ni muhimu kuifahamu vyema falsafa hiyo ya Rais Dkt. Samia na kuitekeleza kwa vitendo. “Nina imani kubwa kwamba uongozi wa juu wa Wizara umeielewa vizuri falsafa hiyo, na semina hii elekezi ni ushahidi tosha wa kuitekeleza kwa vitendo”

Amesema hayo leo (Ijumaa, Septemba 06, 2024) wakati alipofungua Semina elekezi kwa viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Weruweru River Lodge, mkoani Kilimanjaro.

“Falsafa hii inajikita katika masuala ya Maridhiano (Reconciliation), Ustahamilivu (Resilience), Mageuzi (Reforms), na Kujenga upya Taifa (Rebuilding). Hivyo, nitoe wito kwa washiriki ambao ni Maafisa Waandamizi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake kuendelea kushiriki na kuishi kikamilifu falsafa hii”

Ameongeza kuwa semina elekezi hiyo ni sehemu muhimu kwa maendeleo ya kitaaluma na kitaasisi kwa maafisa waandamizi wa vyombo vya usalama, na husaidia katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kufuata viwango vya kitaaluma na kisheria.

“Semina elekezi hutoa fursa kwa maafisa waandamizi kujifunza mbinu na taratibu mpya katika utendaji wa majukumu yao. Hii inajumuisha teknolojia mpya, mbinu bora za ulinzi na usalama, na mbinu za kisasa za kupambana na uhalifu.”

Kwa Upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amemshukuru Rais Dkt. Samia juu ya nia yake ya dhati kwa kufanya maboresho ya Wizara hiyo na vyombo vyake ikiwemo Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto pamoja na Taasisi ya NIDA.

“Maboresho haya yanahusisha upandishaji vyeo wa kihistoria wa Maafisa, Wakaguzi na Askari wapatao 50,971, kuongeza Bajeti ya Miradi ya Maendeleo kutoka mwaka 2021/22 hadi 2024/25 ni Shilingi 262.2 ambayo ni sawa na asilimia 954.59 ya ongezeko la Bajeti ya Miradi ya Maendeleo”

Amesema kuwa Ongezeko hilo la bajeti limesaidia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa vitendea kazi ikiwemo magari, mitambo, boti, vifaa vya TEHAMA na kadhalika.

Previous articleWAZIRI MKUU AFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA VIONGOZI WANDAMIZI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
Next articleSOMA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 7-2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here