Home LOCAL TEF YAPONGEZA KUUNDWA BODI YA ITHIBATI YA WANAHABARI

TEF YAPONGEZA KUUNDWA BODI YA ITHIBATI YA WANAHABARI

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) linawapongeza Mwenyekiti wa Bodi, Tido Mhando na Wajumbe Ndugu Thobias Makoba, Ndugu Kingoba Mgaya, Dkt. Rose Reuben, Dkt. Egbert Mkoko, na Ndugu Ladislaus Komanya kwa kuteuliwa kuunda wajumbe wa Bodi ya Ithibati ya
Wanahabari.

Tunampongeza pia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Slaa aliyefanya uteuzi huu Septemba 18, 2024 na kukamilisha kazi iliyokwamisha utekelezaji wa sheria hii tangu mwaka 2016, yaani miaka minane iliyopita.

Uteuzi huu ulioanza Septemba 18, 2024 utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Ni matumaini yetu kuwa kuteuliwa kwa Bodi ya Ithibati, kutaanzisha mchakato wa kuundwa kwa Baraza Huru la Habari Tanzania (IMCT), ambalo sasa linakwenda kumaliza tatizo sugu la makosa ya kitaaluma kwa wanahabari kupelekwa mahakamani tofauti na taaluma nyingine nchini.

Tunaamini Mwenyekiti na wajumbe walioteuliwa wataifanya kazi hii kwa weledi mkubwa na kwa masilahi ya kukuza taaluma hasa katika kipindi hiki ambacho vyombo vya habari vinachangamoto kubwa ya uchumi.

Tunawatakia kila la heri na kuwaombea katika kazi hii ambayo taaluma ya habari sasa inawekeza matumaini yote kwao.
Mungu ibariki taaluma ya habari, Mungu ibariki Tanzania.

JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)
Deodatus Balile
Mwenyekiti
19/09/2024

Previous articleRAIS DKT .SAMIA AKIAPISHA BAADHI YA VIONGOZI IKULU
Next articleWAZIRI BASHE ATEMBELEA SHAMBA LA KUZALISHA MBEGU ZA SHAIRI RUVUMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here