Home BUSINESS TANZANIA YACHAGULIWA MJUMBE WA BARAZA LA USIMAMIZI WA MADINI YA CHINI YA...

TANZANIA YACHAGULIWA MJUMBE WA BARAZA LA USIMAMIZI WA MADINI YA CHINI YA SAKAFU YA BAHARI KUU

Kingston, Jamaica

Kwa mara ya kwanza Tanzania imechaguliwa kuwa Mjumbe katika Baraza la Usimamizi wa Madini yanayopatikana chini ya Sakafu ya Bahari Kuu katika Mkutano wa Assembly uliofanyika Agosti 02, 2024 jijini Kingston, Jamaica.

Tanzania kuwa mjumbe wa baraza hilo itapata fursa ya kuweka usimamizi madhubuti na endelevu wa madini hayo, kutangaza fursa za madini yanayopatikana Tanzania (Land based minerals) na kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana nchini.

Madini chini ya sakafu ya bahari kuu yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa sehemu ya 11 ya Mkataba wa Usimamizi wa Bahari kuu na makubaliano ya Mwaka 1994 yaani United Nations Convention on the Law of the Sea (UNCLOS) na 1994 Agreement.

Vile vile, Madini hayo yanayosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kuu (InternationalSeabed Authority – ISA) yanatumika katika mabadiliko ya nishati mbadala ya umeme unaopunguza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi na yanapatikana katika kina cha mita kati ya 2000 hadi 6000 chini ya usawa wa bahari.

Katika mkutano huo, Ujumbe kutoka Tanzania uliwakilishwa na wataalam kutoka Wizara ya Madini, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Uvuvi wa Bahari kuu.

Oktoba 2023, Tanzania iliweka historia ya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Sita (6) wa Kimataifa wa Wakandarasi waliowekeza kwenye madini yanayopatikana chini ya sakafu ya bahari kuu ambapo ilipata nafasi ya kujifunza kuhusu utafiti, uvunaji na uendelezaji wa madini hayo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar Es Salaam.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here