Home LOCAL TANZANIA KUJIIMARISHA ZAIDI KIDIPLOMASIA – MAJALIWA

TANZANIA KUJIIMARISHA ZAIDI KIDIPLOMASIA – MAJALIWA

DODOMA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kujiimarisha kidiplomasia na itaongeza nguvu zaidi ili kuwawezesha Watanzania wengi kupata fursa mbalimbali katika jumuia za kimataifa.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikisha kuimarisha ushirikiano baina ya nchi washirika na sasa mafanikio yanaonekana.

“Rais wetu ameonesha nia njema katika kipindi chake cha miaka mitatu na nusu amefanya kazi kubwa ya kujenga diplomasia na mahusiano katika sekta mbalimbali na nchi nyingi duniani.”

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 4, 2024) alipokutana na Mkurugenzi Mkuu Mteule wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika (WHO) Dkt Faustine Ndungulie, Ofisini kwake Mlimwa Jijini Dodoma.

Jitihada hizo za Serikali ya awamu ya sita zimeiwezesha Tanzania kuendelea kupaa kidiplomasia kuiwezesha nchi kupata viongozi wakubwa ndani ya Taasisi za kimataifa.

“Tunaamini kazi kubwa tulizozifanya katika kipindi hiki cha miaka mitatu ya kumpata spika wa Umoja wa Mabunge duniani haikuwa kazi ndogo, na tena tumepata Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika.”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali itaendelea kumuunga mkono Mkurugenzi huyo katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.

“Wakati wote Waziri wa Afya atakuwa karibu nawe kuhakikisha kwamba sera zetu zinaenda sambamba na malengo ya WHO, kwa uwepo wako sisi lazima tuwe msitari wa mbele kuhakikisha kwamba tunakuunga mkono kwa mipango yetu ya afya ndani ya nchi.”

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo Mtarajiwa wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika DKT. Faustine Ndungulile amemshukiru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuunga mkono na kufanya ushawishi wa kidiplomasia ili kufanikisha ushindi huo.

“Kwa upekee sana ninamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake kubwa katika kufanikisha ushindi huu kwa ushawishi wake kwenye jumuia za kimataifa pia nawashukuru viongozi wengine wa Serikali, Bunge na wadau wote.”

Mwisho

 

Previous articleWAKANDARASI MIRADI YA UJENZI YA HEET UDOM WAASWA
Next articleMNADHIMU MKUU WA JWTZ AISHUKURU KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE ULINZI NA MAMBO YA NJE YA SHELISHELI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here