Home BUSINESS RAIS SAMIA KUZINDUA MKUMBI JIJINI DAR

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUMBI JIJINI DAR

Na:  Veronica Mheta, ARUSHA 

RAIS Dk,Samia Suluhu Hassan kesho anatarajia kuzindua taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa mpango wa kuboresha mazingira ya Biashara nchini (MKUMBI) Jijini Dar es Salaam.

Aidha Rais Samia ambaye atawakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, atazindua taarifa ya hali ya uwekezaji nchini ya mwaka 2023, mwongozo wa uanzishaji na uendeshaji wa kanda maalum za kiuchumi nchini, pamoja na mpango mkakati ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

Akizungumza Jijini Arusha na wandishi wa habari , Waziri Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa ,Kitila Mkumbo amesema serikali ilianzisha mpango huo Juni 2019, kwa lengo la kufanya uchambuzi wa kina wa mazingira ya biashara nchini.

Amesema mpango huo ulilenga kuainisha mageuzi na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika kutatua changamoto na kuboresha mazingira ya kufanya biashara pamoja na uwekezaji nchini.

“Mkumbi imefanikiwa kuainisha maeneo makubwa matatu ya kushughulikia uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini, ikiwemo gharama za kufanya biashara,mlolongo mgumu na mrefu wa kupata vibali vya kufanya biashara na uwepo wa utitiri wa mamlaka za udhibiti zinazoratibu shughuli za biashara nchini”

Previous articleMHE. SIMBACHAWENE AMTEMBELEA MAMA SITTI MWINYI
Next articleUGONJWA WA FMD WAJADILIWA KUTOVUKA MIPAKA YA NCHI ZA EAC NA SADC
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here