Home INTERNATIONAL RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA NCHINI CHINA KUANZIA SEPT. 02 -06, 2024

RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA NCHINI CHINA KUANZIA SEPT. 02 -06, 2024

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi Nchini China kuanzia leo September 02 hadi September 06, 2024 kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (Forum on China-Africa Cooperation-FOCAC) utakaofanyika Jijini Beijing.

Taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa B. Nyanga imesema wakati wa ziara hiyo Rais Dkt. Samia atakutana na Mwenyeji wake Rais wa China, Xi Jinping, kwa mazungumzo yanayolenga kuimarisha uhusiano mzuri na wa kihistoria kati ya Tanzania na China ulioasisiwa miaka 60 iliyopita.

Marais hao wawili pamoja na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema watashiriki na kushuhudia uwekaji saini wa Hati za Makubaliano ya Uboreshaji wa Reli ya TAZARA.

Pamoja na mambo mengine, miongoni mwa maeneo yanayotarajiwa kupewa kipaumbele kwenye Mkutano wa FOCAC ni uendelezaji wa miundombinu, kukuza uwekezaji, uendelezaji wa viwanda, kilimo cha kisasa na amani na usalama, Rais Dkt. Samia anatarajia kuwa miongoni mwa Wakuu wa Nchi watakaohutubia ufunguzi wa Mkutano wa FOCAC akizungumza kwa niaba ya Kanda ya Afrika Mashariki.

Pembezoni mwa mkutano huo, katika kukuza biashara na uwekezaji, Rais Dkt. Samia atakutana na makampuni na Wawekezaji kutoka China kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji zaidi Nchini Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here