Home INTERNATIONAL RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS XI JINPING WA CHINA

RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS XI JINPING WA CHINA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping katika ukumbi wa The Great Hall of the People kabla ya kuanza mazungumzo jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.
BEIJING – CHINA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mkutano na Rais wa China, Xi Jinping pamoja na ujumbe wake mapema leo katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing.

Rais Samia amefanikiwa kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ya Tanzania na nchi muhimu duniani ikiwepo China tangu alipoingia madarakani Mwaka 2021.

Kwa Mwaka huu wa 2024 Rais Samia na Xi Jinping wamejadiliana kuimarisha uhusiano wetu mzuri uliodumu zaidi ya miaka 60.

Vilevile baada ya kikao hicho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping pamoja na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema walishuhudia uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya kuboresha reli ya TAZARA.

 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping pamoja na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakishuhudia uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya kuboresha reli ya TAZARA katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.

   

Previous articleRAIS SAMIA AZUNGUMZA NA RAIS WA CHINA XI JINPING 
Next articleWAKANDARASI MIRADI YA UJENZI YA HEET UDOM WAASWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here