Home BUSINESS PPRA YAWEZESHA KUSOMANA KWA MIFUMO ZAIDI YA 17 NCHINI

PPRA YAWEZESHA KUSOMANA KWA MIFUMO ZAIDI YA 17 NCHINI

Na Veronica Mheta, Arusha

MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma(PPRA) imewezesha kusomana kwa mifumo zaidi ya 17 iliyopo nchini kupitika mfumo mpya wa kieletroniki wa NeST kwenye sekta ya ununuzi wa umma .

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPRA ,Denis Simba wakati akiongea na waandishi wa habari juu Kongamano la 16 la Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki linaloanza Septemba 9-12 Jijini Arusha na kushirikisha washiriki zaidi ya 500.

Amesema kupitia mfumo wa NeST umewezesha sekta ya manunuzi kuimarika zaidi katika usawa uwazi na ushindani katika sekta ya manunuzi .

“PPRA ni kinara wa mfumo wa NeST unaosimamia manunuzi na imefanikiwa kunganisha mifumo zaidi ya 17 kupitia mfumo wa kieletroniki na Tanzania ni kinara katika kutekeleza na kusimamia ununuzi wa kidigitali “.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here