Home LOCAL MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MHE.HAMZA JOHARI AMEWASILISHA MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO...

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MHE.HAMZA JOHARI AMEWASILISHA MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO BUNGENI

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari amewasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2024 [ The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 2) Bill, 2024], Muswada huo umewasilishwa mbele ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania tarehe 3 Septemba, 2024, Bungeni Jijini Dodoma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema Muswada huo unalenga kufanya Marekebisho katika Sheria kuu nane ambazo ni; Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu Sura ya 432 ( The Anti- Trafficking in Person Act, Cap 432), Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura ya 20 ( The Criminal Procedure Act, Cap 20), Sheria ya Serikali Mtandao Sura ya 273 (The e-Government Act, Cap 273) Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 ( The Immigration Act, Cap 54), Sheria ya Ardhi Sura ya 113 (The Land Act, Cap 113), Sheria ya Bohari ya Dawa 70 ( The Medical Stores Department Act, Cap 70) Sheria ya Viwango Sura 30 ( The Standard Act, Cap 30) na Sheria ya Tume ya Mipango Sura ya 127 ( The Planning Commission Act, Cap 127).

Akiwasilisha Muswada huo Mhe. Johari amesema Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu Sura ya 432, ambayo ilitungwa Mwaka 2008 na mpaka sasa imeshafanyiwa marekebisho mara 5, amevitaja vifungu vilivyopendekezwa kufanyia marekebisho katika sheria hiyo kuwa ni kifungu cha 3,17,30 31 32, vilevile Sheria hiyo inapendekeza kuongezwa kwa vifungu vipya vya 24A, 24B, 24C, na 24D.

“Mhe. Naibu Spika marekebisho yaliyopendekezwa yanalenga kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa vifungu mbalimbali wa sheria hii na kuboresha vifungu hivyo ili kuimairisha Nyanza zote za kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu”.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameendelea kueleza kuwa Sheria ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura ya 20, Sheria hii ilitungwa mwaka 1985 mpaka sasa imeshafanyiwa marekebisho mara 35, kifungu kinachopendekezwa kurekebishwa ni kifungu cha 205A kwa kuanisha namna muundo wa kuandaa ripoti ya uchunguzi wa Kifolensiki

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here