Home LOCAL MONGELA AKABIBIDHIWA TAARIFA YA UTEKELEZAJI MRADI WA MAJI USHETU

MONGELA AKABIBIDHIWA TAARIFA YA UTEKELEZAJI MRADI WA MAJI USHETU

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, alikabidhiwa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa skimu ya maji kutoka kijiji cha Nyankende hadi kijiji cha Mwadui, Halmashauri ya Ushetu, mkoani Shinyanga, tarehe 8 Septemba 2024.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama, Mhandisi Maduhu Magili, alieleza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi huu wa Septemba 2024. Lengo kuu ni kutatua tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji cha Mwadui, sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita za kumtua mama ndoo kichwani.

Chanzo cha maji kwa mradi huo ni kisima kirefu kilichopo kijiji cha Nyankende, chenye uwezo wa kuzalisha lita 14,000 kwa saa. Mradi huu, ukiwa umekamilika kwa asilimia 85, utahudumia takriban wakazi 2,058 wa kijiji cha Mwadui na unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 300.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here