Home LOCAL MHE. SIMBACHAWENE AMTEMBELEA MAMA SITTI MWINYI

MHE. SIMBACHAWENE AMTEMBELEA MAMA SITTI MWINYI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Mama Sitti Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam Septemba 10, 2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amemtembelea Mama Sitti Mwinyi nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo Septemba 10, 2024. 
 
“Rais, amenielekeza kuwafikishia salaam zake na amesema yuko pamoja nanyi na ndio mana amenituma kufika hapa nyumbani na kuwajulia hali, kusikiliza changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi” amesema Mhe. Simbachawene.
 
Mhe. Simbachawene amesema Rais Mhe. Dkt. Samia anathamini sana mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa waliomtangulia na ataendelea kusimamia na kutunza familia hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria.
 
Aidha, Mama Sitti amemshukuru Mhe. Simbachawene kwa kupata nafasi ya kumtembelea na kumjulia hali na amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia yake wakati wote bila kuchoka na amemuombea kwa Mungu aendelee kutumia hekima na busara katika kuiongoza Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene wakifuatilia jambo na Mama Sitti Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam Septemba 10, 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na Mama Sitti Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam Septemba 10, 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Mama Sitti Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam Septemba 10, 2024
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na Mama Sitti Mwinyi wakati alipomtembelea nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es Salaam Septemba 10, 2024
Previous articleSUALA LA MAZINGIRA LIWE AJENDA YA KITAIFA-MHE.KASSIM MAJALIWA
Next articleRAIS SAMIA KUZINDUA MKUMBI JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here