Home LOCAL MHE.HUSSEIN BASHE AIPONGEZA KAMPUNI YA GAKI

MHE.HUSSEIN BASHE AIPONGEZA KAMPUNI YA GAKI

Kampuni ya GAKI Investment Ltd. inayomilikiwa na Bw. Gaspar Kileo, Mkurugenzi yapongezwa kwa uwekezaji mzuri wenye tija kwa kuwa mwekezaji na mnunuzi wa Pamba ambazo Kata tatu za Mbutu, Kishapu na Meatu zinazalisha.

Pongezi hizo zimetolewa na Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho tarehe 12 Septemba 2024, mkoani Shinyanga. “Kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba, mmekuwa mfano mzuri wa kuajiri Maafisa Ugani 15 chini ya mpango wa BBT Ugani kwa kuwezesha wakulima wa kata hizo tatu kunufaika na elimu ya kilimo bora cha Pamba na kuongeza mavuno yenye tija kutoka kilo 200 hadi 1000 kwa ekari,” amesema Waziri Bashe.

Waziri Bashe ameeleza kuwa utararibu huo wa kutumia Maafisa Ugani wa BBT Ugani umeonesha manufaa hususan kufuatia Viwanda vinavyochambua zao la Pamba ikiwemo kampuni ya GAKI kuonesha kufurahishwa na mpango huo kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba.

Utararibu wa kutumia Maafisa wa BBT Ugani kwa zao la Pamba umehusisha kusambaza maafisa ugani 5 ambapo kila kijiji kuna Afisa Kilimo mmoja ili kutoa huduma za Ugani kwa wakulima. Aidha, programu ya BBT Ugani ambayo ina wahitimu 230 ilianzishwa msimu uliopita kwa lengo la kila zao kuwa na utaratibu kama huu wa zao la Pamba katika kuwezesha huduma za ugani kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji wenye tija.

Serikali imetoa trekta kwa lengo la kila kijiji hatimae kuwe na trekta 2 ili kusaidia shughuli za kilimo kwa wakulima. Ruzuku za mbolea na mbegu zitaendelea kuwepo kwa matumizi bora ya kilimo, huku huduma za ugani zikiongezwa,” amesema Waziri Bashe.

Ziara pia imeshirikisha viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya ya Shinyanga akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamiringi Macha, na Wawakilishi kutoka Wizara ya Kilimo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here