Home LOCAL MHE.CHALAMILA AMEPOKEA TAARIFA YA KAMATI ALIYOIUNDA YA    SOKO LA KARIAKOO

MHE.CHALAMILA AMEPOKEA TAARIFA YA KAMATI ALIYOIUNDA YA    SOKO LA KARIAKOO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Septemba 04, 2024 amepokea taarifa ya kamati aliyoiunda kupitia orodha ya majina ya wafanyabiashara wa soko la Kariakoo katika ukumbi wa mikutano Arnatoglo Mnazi mmoja-Ilala.
RC Chalamila akipokea taarifa hiyo amesema alilazimika kuunda kamati hiyo ili kujiridhisha juu ya mchakato mzima uliotumika kupata orodha ya majina ya awali ya wafanyabiashara hao kutokana na unyeti wa eneo la soko la Kariakoo kwa masilahi mapana ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Aidha kikao hicho kimehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Bi Hawa Ghasia, Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo, Mkurugenzi wa Jiji Bwana Elihuruma Mabelya pamoja na wajumbe wa kamati wakiongozwa na mwenyekiti wa Kamati Mhandisi Amani mafuru.
Mwisho RC Chalamila ameipongeza kamati hiyo kwa kazi nzuri, hatimaye baada ya kupokea ripoti hiyo alipata wasaa wa kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wajumbe kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here