Home LOCAL MHE.BASHE ATANGAZA NEEMA SEKTA YA UMWAGILIAJI SHINYANGA

MHE.BASHE ATANGAZA NEEMA SEKTA YA UMWAGILIAJI SHINYANGA

Waziri wa Kilimo Mhe. Husein Bashe (mb) ametembelea mradi wa Umwagiliaji wa Nyida uliopo mkoani Shinyanga wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kuelekeza kuwa ndani ya mradi huo lijengwe ghala kubwa la kuhifadhi mpunga.

Waziri Bashe ameelekeza ufanyike ujenzi wa kituo cha pamoja cha kununua mpunga na kufungwa mashine na kinu cha kuchakata mchele, sambamba na ujenzi wa barabara ya uhakika yenye urefu wa km 7.5 itayoungana na barabara kubwa ya lami na kujenga pamoja na kujenga Mabirika kunyweshea wanyama.

Waziri Bashe amesema hayo katika muendelezo wa ziara yake akiwa anakagua mradi wa Nyida uliopo mkoani Shinyanga.

Aidha Waziri Bashe ameelekeza kuongezwa kwa mradi mdogo wa Nyida wenye hekta zaidi ya 400 na skimu hiyo itangazwe hivi karibuni.

Amesisitiza kuwa skimu ya Nyida yenye hekta 400 itangazwe ili ipate mkandarasi na aanze kujenga ili wananchi wanufaike.

Amesema, anatambua rasiliamali fedha ni chache lakini Dkt.Rais ameamua kutenga fedha za ujenzi wa miradi hiyo itakayohudumia halmashauri mbili ambayo ni Nzega Dc na Shinyanga vijijini.

Waziri Bashe, amesisitiza kuwa bwawa hilo lenye ujazo Mita za ujazo milioni 7 na mfumo wa kutoa maji yanapojaa itasaidia kuepuka maji yanayofurika na kuharibu miundombinu ya barabara.

Amesema ujenzi wa miradi hiyo iliyoanza Nyida pekee serikali inatumia fedha za walipa kodi zaidi ya sh.Bilioni 55 sawa na vituo vya afya 100, ambapo ingejengwa barabara za lami ni zaidi ya km 50.

Ameeleza kutokana na hatua hiyo ujenzi huo ufanyike kwa kiwango kinachotarajiwa na utunzwe kwa maslahi ya wananchi wa Shinyanga na Taifa kwa ujumla.

Waziri Bashe amesema Rais Dkt. Samia ameamua kuboresha sekta ya kilimo, kutoa ruzuku za mbolea, mbegu, ruzuku za maindi na nyingine kwa lengo la kuinua wakulima kiuchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NIRC Raymond Mndolwa, amesema Tume inaendelea na mpango wa kujenga mabwawa, kukarabati skimu za zamani na kuibua maeneo mapya kwa ajili ya kilimo.

Mndolwa amesema ujenzi wa bwawa la Nyida ulianza mwaka 2023 na unatarajiwa kukamilika April mwakani ambapo hadi sasa umefikia asilimia 68, ukijumuisha ujenzi wa mabwawa ya Katunguru Sengerema Mwanza na Kasoli,Bariadi Simiyu yote matatu yakiwa na gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 29.

Aidha kwa mwaka wa fedha 2024/2025 serikali kupitia Tume imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa mabwawa saba na katika mabonde ya Lunguya, Mwamkanga, Amani, Ngaganulwa, Nimbo, Bulungwa na Kisuke.

Previous articleBASHE: UTAFITI NA UZALISHAJI WA MBEGU BORA HUCHANGIA TIJA KWENYE KILIMO
Next articleBoT, AZAKI WAJADILI KUBORESHA HUDUMA JUMUISHI ZA FEDHA KWA JAMII

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here