Home BUSINESS MATUMIZI YA TEKNOLOJIA MBADALA YAPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI: MHANDISI MATIVILA

MATUMIZI YA TEKNOLOJIA MBADALA YAPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI: MHANDISI MATIVILA

DAR ES SALAAM

Matumizi ya Teknolojia mbadala na malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja imeweza kupunguza gharama zaidi ya asilimia 70.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila alipotembelea banda la TARURA kwenye Maadhimisho ya 21 ya Siku ya Wahandisi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“Ujenzi wa madaraja na barabara kwa kutumia teknolojia ya mawe unapunguza gharama kwa asilimia 70 ukilinganisha na zege lakini pia tuna teknolojia ya kutumia kemikali kuboresha udongo unaopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi”, amesema.

Ameongeza kwamba TARURA imeweza kuondoa vikwazo sehemu zisizopitika kwa kujenga madaraja ya gharama nafuu kwa kutumia teknolojia mbadala hasa maeneo ya vijijini na kuwezesha wananchi kuzifikia huduma za kijamii na kiuchumi kwa urahisi zaidi.

“Kwa bajeti ya shilingi bil. 1 unayoweza kujenga daraja 1 unajenga madaraja 3 ya mawe, lakini pia ukitumia udongo unaopatikana maeneo ya kazi unakuwa umepunguza gharama na mtandao mkubwa wa barabara hasa za vijijini ambapo kuna uzalishaji mkubwa wa mazao unakuwa unapitika katika Kipindi chote cha mwaka”.

Previous articleWIZARA YA NISHATI ENDELEENI KUUSIMAMIA MRADI WA JNHPP IPASAVYO KAMATI YA BUNGE
Next articleGRASSLAND RESTORATION AND MANAGEMENT STRATEGIES IN HULUN-BUIR, INNER MONGOLIA: LESSONS FOR TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here