Home LOCAL DKT. BITEKO AKUTANA NA BALOZI MPYA WA UINGEREZA NCHINI

DKT. BITEKO AKUTANA NA BALOZI MPYA WA UINGEREZA NCHINI

*Tanzania na Uingereza Kuimarisha Ushirikiano katika Sekta ya Nishati*

*Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati*

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko Septemba 6, 2024 jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na balozi mpya wa Uingereza nchini. Mhe. Marianne Young.

Lengo la mazungumzo hayo likiwa ni kujitambulisha kwa balozi huyo pamoja na kujadili masuala ya kipaumbele ya ushirikiano baina ya Tanzania na Uingereza katika sekta ya nishati.

Aidha katika mazungumzo hayo, Dkt.Biteko amepongeza ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Uingereza katika sekta mbalimbali hususan sekta ya nishati kupitia ufadhili wa fedha kiasi cha shilingi bilioni 11.16 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Songas kupitia taasisi zake za mitaji za Shirika la UK Export Finance (UKEF) na Shirika la Uwekezaji la Uingereza (BII).

‘‘Serikali itaendelea kushirikiana nanyi katika sekta ya nishati sambamba na kuikaribisha sekta binafsi kutoka nchini Uingereza kuja kuwekeza Tanzania katika uzalishaji, uhifadhi na usambazaji wa nishati hususan nishati safi ya kupikia na nishati mbadala, ’’ amesema Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Balozi Young, ameipongeza Tanzania kwa uongozi wake katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika na kusema kuwa nchi yake itaendelea kuunga mkono sekta ya nishati nchini.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Denis Londo.

MWISHO.

Previous articleSOMA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 7-2024
Next articleWAZIRI MKUU ASHIRIKI MBIO ZA HISANI JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here