Uongozi wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Lindi umewataka viongozi wote kuzitumia mali za chama kwa ajili ya kukijenga chama na sio kwa ajili ya shughuli za mtu binafsi.
Akizungumza na mwandishi wetu Katibu wa CCM Mkoa wa Lindi Barnabas Essau (MNEC) amewataka viongozi wa CCM mkoa wa Lindi kulinda na kuzitumia mali za chama hicho ili zisaidie katika shughuli mbalimbali za kukijenga chama hicho.
Katibu Essau ametoa kauli hiyo akiwa katika jimbo la kilwa Kaskazini ambapo amewataka watendaji wa CCM na Jumuiya zote wadhibiti wa Mali za Chama wahakikishe mali zote zinatumika kwa shughuli za ujenzi wa Chama na siyo vinginevyo maana mali hizo ni za Chama na siyo mtu binafsi hivyo Viongozi wote wana haki ya kuzitumia hasa pale wanapofanya shughuli za ujenzi wa Chama.
Sambamba na hilo Essau amewataka Viongozi wa kata zote wahakikishe Wanachama na Wananchi wanajitokeza Kwa wingi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la wakazi ili waweze kushiriki Kwa ukamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji na kuhakikisha wale Wanachama wote wenye sifa wajiandae kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa ,Vijiji na Vitongoji wakati utakapofika.
Imetolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Lindi.