Home BUSINESS WAZIRI NDEJEMBI AITAKA NHC KUWASAIDIA WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI KUMILIKI NYUMBA

WAZIRI NDEJEMBI AITAKA NHC KUWASAIDIA WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI KUMILIKI NYUMBA

DAR ES SALAAM 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi, amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),  kuende;eza mikakati yake ya kuwasaidia wananchi mwenye kipato cha chini kumiliki nyumba.

Waziri Ndejembi ameyasema hayo leo Agosti 9,2024 alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa malengo ya kuanzishwa kwa  Shirika hilo lililoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere ni kujenga nyumba zenye viwango vya  hali ya juu ambazo pia zinaweza kununuliwa na wananchi wenye kipato cha chini.

Amesema kuwa NHC inapaswa kuanzisha utaratibu wa kulipa kiasi fulani cha asilimia ya gharama ya Nyumba na kuruhusu mteja huyo kuanza kuishi huku akiwa analipa kiasi kidogo cha fedha kila mwezi mpaka atakapomaliza deni lake.

Aidha, Mhe. Ndejembi amelipongeza  Shirika hilo  kwa kuanza utekelezaji wa mradi wa Samia Housung Scheme wenye lengo la kujenga Nyumba 5,000, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mradi huo katika maeneo  ambayo bado hayafikiwa na yenye uhitaji.

Mhe. Ndejembi ametoa wito kwa menejimenti ya NHC kuhakikisha hakuna wizi wa vifaa vya ujenzi wakati wa utekelezaji wa miradi ya Shirika nakwamba kwa kufanya hivyokutasaidia  thamani ya Nyumba kuendana na gharama halisi za ujenzi.

Previous articleRAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA JENGO LA MAABARA KUU YA KILIMO
Next articleGLOBAL EDUCATION LINK YATOA VISA 100 KWA WANAOENDA KUSOMA NJE YA NCHI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here