Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) akiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Sempeho Manongi na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo Bw. Needpeace Wambuya amekutana na kuzungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe.Balozi Marianne Young katika 0fisi ya Wizara, jijini Dodoma.
Mhe. Jafo amesema kuwa wamejadiliana kuhusu namna ya kuimarisha Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji baina ya nchi hizo.