Home BUSINESS WAZIRI JAFO ATAKA KILA MKOA KUANZISHA VIWANDA

WAZIRI JAFO ATAKA KILA MKOA KUANZISHA VIWANDA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Selemani Jafo,akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akiitambulisha Programu ya utekelezaji Programu ya Viwanda (2025- 2026) inayoongozwa na Kauli mbiu isemayo “Viwanda vyetu, Ajira zetu Uchumi wetu” leo Agosti 15, 2024 jijini Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Selemani Jafo,akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 15, 2024 jijini Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Selemani Jafo ameiagiza Mikoa yote Tanzania Bara kuanzisha viwanda ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Viwanda (2025 – 2030) kwa lengo la kutengeneza ajira na kukuza uchumi kwa ujumla.

Badilisha ni Programu ya Viwanda 2025- 203 tafadhali samahani

Dkt Jafo ameyasema hayo katika Mkutano na Waandishi wa Habari wakati akiitambulisha Programu hiyo inayoongozwa na Kauli mbiu isemayo “Viwanda vyetu, Ajira zetu Uchumi wetu” uliofanyika Agosti 15, 2024 jijini Dodoma

Akielezea utekelezaji wa Programu hiyo, Dkt Jafo amebainisha kuwa kila Mkoa unapaswa kuanzisha Viwanda vikubwa 3, Viwanda vya kati 5, Viwanda vidogo 20 na Viwanda vidogo sana 30 ambapo kwa mwaka mikoa hiyo itakuwa na jumla ya Viwanda vikubwa 78 Viwanda vya kati 130, Viwanda Vidogo 520, Viwanda vidogo sana 780 na jumla ya viwanda vyote 1,508 kwa mwaka ambavyo vitazalisha ajira za moja kwa moja 173,160 na ajira zisizo za moja kwa moja 911,300 kwa mwaka.

Vile vile amesema kuwa katika kipindi hicho cha 2025-2030 kupitia programu hiyo kutakuwa na Jumla ya Viwanda vikubwa 468, Viwanda vya kati 780, Viwanda vidogo 3120, Viwanda Vidogo sana 4,680 na jumla ya viwanda vyote 9,048 vitakavyozalisha ajira za moja kwa moja 1,038,960 na zisizo za moja kwa moja 5,467,800.

Dkt. Jafo pia amebainisha sekta zitakazohusika na Programu hiyo kuwa ni pamoja na Madini, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Nishati, Mawasiliano, Ujenzi, Afya, Maliasili na Misitu, Elimu, Biashara za Huduma(Taasisi za Fedha, hotel, n.k} pamoja na Uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kama vile nguo, saruji, chuma, marumaru.

Aidha, amebainisha kuwa Programu hii itahusisha Taasisi mbalimbali za umma, sekta binafsi vyombo vya habari, pamoja na Viongozi mbalimbali kianzia ngazi ya Halmashauri hadi Serikali Kuu

Aidha, amesema Tathimi ya utekelezaji wa Programu hiyo kwa kila Mkoa na Mkoa utakaofanya vizuri utazawadiwa zawadi maalumu kama motisha ikiwemo Kombe (Samia Industrial Award), kupewa kipaumbele katika kuwezesha utekelezaji wa Programu hiyo pamoja na kufanya utalii wa ndani katika moja ya vivutio kwa mshindi wa kila mwaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here