Home BUSINESS WATEJA WA DAWASA JAZENI FOMU YA EWURA e-LUC KUBORESHA HUDUMA

WATEJA WA DAWASA JAZENI FOMU YA EWURA e-LUC KUBORESHA HUDUMA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imewataka wateja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kujaza fomu maalum (EWURA e-LUC) ili kuiwezesha EWURA kufuatilia utendaji wa mamlaka hiyo katika kuwahudumia wateja wake.

Mfumo wa EWURA e-LUC unalenga kupata taarifa za kiwango ambacho wateja wa mamlaka za maji nchini wanahudumiwa na kufahamishwa kuhusu haki zao za msingi kulingana na Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa mamlaka ya maji husika ili kubaini hali ya huduma ilivyo na kuchukua hatua stahiki.

Kwa kuanzia, EWURA inatumia mfumo huu (EWURA e-LUC) kupata mrejesho kutoka kwa wateja wa DAWASA.

Hivyo basi, wateja wa DAWASA wanaombwa kujaza fomu maalumu ya EWURA e-LUC kwa kubofya kiunganishi (link) https://forms.gle/94vdRu87yQ1rWwKs6 ili kuweka taarifa zinazohusu huduma mbalimbali zinazotolewa na mamlaka hiyo ya maji.

Previous articleTANZANIA KUSHIRIKIANA NA CUBA UTAFITI WA MIMEA TIBA-MAJALIWA
Next articleWAZIRI MKUU KASIMU MAJALIWA AKIFANYA ZIARA MAALUM KUBORESHA MAHUSIANO KATI YA CUBA NA TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here