Home Uncategorized WATAFITI WAUNDA CHAMA CHA KISAYANSI CHA ‘ATARE’ KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI

WATAFITI WAUNDA CHAMA CHA KISAYANSI CHA ‘ATARE’ KUCHANGIA UKUAJI WA UCHUMI

Watafiti nchi wameunda chama kinachoitwa ATARE kuunganisha tafiti mbalimbali za kisayansi za wataalamu na kuona umuhimu na michango ya utafiti katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Hayo yamebainishwa Agosti 8, 2024 na    Prof. Joseph Ndunguru  Wakati wa kilele cha Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Amesema hakuna inchi inayoweza kufanikiwa bila utafiti hivyo wanataka michango ya utafiti iweze kuonekana na ikuze uchumi wa nchi ya Tanzania.

“Chama hiki cha ATARE kimeanzishwa  mwaka Jana, kimesajiliwa chini ya sheria ya mashirika yasiyo yakiserikali ya mwaka 2002 na ni chama ambacho kinaunganisha watafiti wote wa fani mbalimbali ikiwemo kilimo,mifugo na madini”, amesema

Amesema wanataka watafiti wa Tanzania kuwaunganisha na Taasisi za utafiti za nje ili kufanya vitu viwili ikiwemo kuwatambulisha pamoja na kuwatafutia fedha kwaajili ya kufanya utafiti.

“Tunataka kuanzisha kanzi data za utafiti wote uliofanyika Tanzania kwa ajili ya matumizi ya Sasa hivi na vizazi vijavyo,pia tutakuwa na machapisho mbalimbali kwa ajili ya watafiti kuweza kusambaza matokeo ya utafiti wao kwa wadau,tunataka tutumie chama hiki kuwahamasisha vijana walioko kwenye vyuo mbalimbali waweze kujihusisha na utafiti na tutawalea ili waje wawe watafiti wabobezi katika fani zao.”Amesema Profesa Ndunguru.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here