Home BUSINESS UDOM WAFANIKIWA KUBUNI MIFUMO YA TEHAMA

UDOM WAFANIKIWA KUBUNI MIFUMO YA TEHAMA

Michael Mmassi Mwanafunzi mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha UDOM anayesoma utaalam wa Mifumo ya mawasiliano.

Neema Mchanga mkufunzi msaidizi Chuo Kikuu cha Dodoma UDSM akielezea mfumo wa kilimo cha umwagiliaji. 

DODOMA

Chuo Kikuu Cha Dodoma wemefanikiwa kubuni mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yenye lengo la kuwasaidia wakulima ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi katika uzalishaji wa mazao.

Akizungumza leo Agosti 6, 2024 katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika Nzuguni jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Cha Dodoma Bi. Rose Joseph, amesema kuwa mifumo hiyo ya TEHAMA imebuniwa na wanafunzi wa Chuo hicho ili kuhakikisha wanatoa mchango kwa wakulima katika utekelezaji wa majukumu yao

Bi. Joseph amesema kuwa katika maonesho hayo wamekuja na mifumo zaidi mitatu ya Teknolojia ikiwemo mfumo wa kubaini maradhi ya mimea kama maharage.

“Teknolojia hii inasaidia kuangalia zao la maharage limepata maradhi ya aina gani
ili kupata dawa ambayo itasaidia kuzalisha mazao mengi” amesema.

Amesema kuwa pia wamebuni teknolojia kubaini wadudu ambao wanashambulia matiti ya Ng’ombe, hivyo mfumo huo utasaidia kudhibiti mapema wadudu hao na kusaidia uzalishaji wa lita nyingi za maziwa.

“Pia tumebuni teknolojia ambayo imelenga kuwasaidia wakulima ambao wapo katika maeneo ambayo hakuna nishati ya umeme hasa vijijini, mfumo huu unatumia upepe ambao unaweza kuchaji betri na kupata nishati ya kuendesha mitambo ya umwagiliaji wakati wote kadri unavyotaka” amesema Bi. Joseph.

Bi. Joseph amewakaribsha wadau wa sekta ya kilimo katika banda lao kwa ajili ya kuangalia Teknolojia hizo na kushauri maboresho kwa ajili uhitaji wao kadri inavyowezekana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here