Kaimu Meneja Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Kutoka Dodoma jiji Mhandisi Kasongo J. Molijo ameeleza changamoto wanayoipata Kutokana na wananchi kutupa taka hovyo kwenye mitaro na mitaro hiyo kuziba.
Akizungumza katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nanenane) yanayoendelea kwenye viwanja vya Njuguna jijini Dodoma amesema kuna baadhi ya watumiaji wa barabara watembea kwa miguu pia watumiaji wa vyombo vya moto wamekuwa wakitumia barabara vibaya.
“Sisi Kama TARURA tunapitia changamoto kubwa Sana kutokana na wananchi kutupa taka kwenye mitaro na kusababisha maji ya mvua kusimama na kujaa barabarani hiyo hupelekea mitaro hiyo kuziba na barabara kuwa chafu.
TARURA inawajibika kuzibua mitaro hiyo kutokana na taka zilizojaa mitaroni, baadhi ya wananchi wamekuwa wakijenga nyumba kando kando ya barabara hivyo husababisha wananchi jambo ambalo linapelekea TARURA kuwaondoa barabarani na wengine kulipwa fidia.
Amesema kuwa TARURA inazidi kupambana na ujenzi wa barabara ambapo kuna miradi mingi inayoendelea sasa hivi ikiwemo miradi midogo ya matengenezo na miradi mikubwa ya barabara za lami,lengo la ujenzi wa miradi hiyo ni kuhakikisha maeneo mengi nchini kufikika kirahisi na jamii ili kupata huduma
Tuna barabara ambayo inajengwa kutoka Kisima cha nyoka kwenda mpaka Nkuhungu ili kuhakikisha wananchi kutoka Nkuhungu wanafika mjini kiurahisi bila kuwa na kikwazo cha aina yoyote. ” Mhandisi Kasongo J. Molijo.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Bi. Catherine Sungura ameongeza kuwa TARURA inawafahamisha wananchi na kuwapa elimu jinsi tunavyojenga na kutengeneza miundombinu ya Barabara ikiwemo mifereji ya maji.
TARURA imeweza kuwasaidia wakina akitolea mfano wajawazito kutokana na kujenga barabara sehemu ya vijijini na kazi kubwa Sana imefanyika hasa vijijini.
Hii imewasaidia wananchi katika kufanya shughuli zao na kuwasaidia katika kupata huduma kwa haraka”.amesema.