Home BUSINESS MSAJILI WA HAZINA AIPONGEZA TAZAMA KWA KUTOA GAWIO LA SH. BIL ION4.35...

MSAJILI WA HAZINA AIPONGEZA TAZAMA KWA KUTOA GAWIO LA SH. BIL ION4.35 KWA SERIKALI

Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko – watatu kulia, akipokea gawio kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati wa Zambia na Mwenyekiti Bodi ya TAZAMA, Peter Mumba -wa pili kulia, katika hafla iliyofanyika leo Agosti 26,2024 Jijini Dar es Salaam.

Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla ya utoaji wa gawio hilo iliyofanyika leo Agosti 26,2024 Jijini Dar es Salaam.

Na; Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM 

Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu amelipongeza Shirika linalosimamia Bomba la Mafuta kutoka Tanzania kwenda Zambia (TAZAMA). kwa kutoa gawio la Sh. Bilioni 4.35 kwa Serikali ya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni takribani miaka 15 iliyopita tanguilipota gawio la mwisho kwa Serikali.

Amesema utolewaji wa gawio hilo unaakisi moja kwa moja farsafa za R4 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Ujenzi mpya.

Mchechu amesema hayo katika hafla ya utoaji wa gawio hilo iliyofanyika leo Agosti 26,2024 Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko aliyekuwa mgeni rasmi.

“Umri huo kama mtumishi wa umma amebakiza miaka miwili kustaafu, anakuwa kidogo mnyonge mnyonge lakini kwa Tazama badala ya kuwa mnyonge ndio imekuja juu, imekuwa tofauti kidogo.

“Kinachofanyika leo kimetutia faraja kubwa sana, Shirika la TAZAMA lilianza miaka 58 iliyopita katika miaka miaka hiyo ingekuwa ni umri wa mtu anakuwa na miaka miwiili kabla hajastaafu, lakini Tazama imeanza kuamka na nguvu kubwa ikiwa na miaka hiyo 58“  Amesema Mchechu.

Akifafanua zaidi amesema kuwa Shirika hilo ukiaacha kile kipindi cha mwaka 2019 wana miaka 15 ambayo wana hisa hawajapata Gawio, lakini katika mababadiliko ambayo yanasimamiwa nanchi hizo mbili na viongozi wake na kwa upande wetu Tanzania mageuzi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia  Makatibu wakuu wake  katika utekelezaji wameona  manufaa yake na hivyo anamshukuru Mhe. Rais namna ambavyo wametekeleza na kuziishi hizi 4R kwa kiwango cha juu.

Aidha, ameipongeza TAZAMA, nakwamba faida waliyoanza nayo sio tu wameizalisha kwa mwaka mmoja, lakini ni faida ambayo ni kubwa kwa mpigo katika kipindi cha mwaka mmoja ambao hawajawahi kuzalisha lakini wamepata faida ya Sh.Bilioni 52.25, kwa hiyo wameanza kwa kishindo na kishindo chao ni kikuu kimesikika.

“Mheshimwa Waziri Mkuu, gawio kama hili ambalo tumepata leo tunawashukuru sana TAZAMA, nakama ulivyoelekeza fedha hizo ziende kwenye miradi ninasema itakwenda, na nafikiri tutaendelea kupata gawio kubwa zaidi“ amesema

Amesisitiza Kiwango kilichopatikana cha Bilioni 4.35 ni kikubwa kwa taasisi ambayo ilikuwa inasuasua.

“Nawapongeza TAZAMA kwa hatua hii waliyofikia, nawahimiza  kuendeleza juhudi mlizozianzisha ili mwaka ujao mfanye vizuri zaidi amesema.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here