Home BUSINESS NIC YATAMBULISHA BIDHAA MPYA ‘BIMA YA MAISHA’ KWA WAKUU WA TAASISI ZA...

NIC YATAMBULISHA BIDHAA MPYA ‘BIMA YA MAISHA’ KWA WAKUU WA TAASISI ZA SERIKALI

Arusha

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limezindua bidhaa mpya ya Bima ya Maisha itakayo mnufaisha muhusika pamoja na wategemezi wake pale atakapopata janga la kifo.

Uzinduzi huo umefanyika na kutambulishwa rasmi Agosti 30,2024 Jijini Arusha kwa wakuu wa taasisi na Wakuruguenzi wa kampuni mbalimbali  wakati wa Kikao maalum cha wakuu hao kilichofanyika Jijini humo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa NIC  Kaimu Abdi Mkeyenge,  amesema bidhaa hiyo inakwenda kuwasaidia wakuu hao na wananchi wote pale wanapo ondokewa na watu wao wa karibu katika familia.

Amesema Bima hiyo tayari ipo sokoni na NIC imeleta bidhaa hiyo ili kuongeza wigo na upana wa shughuli zake Kibiashara.

“Tumeamua kuelezea umuhimu wa Bima hii ili kuwasaidia wakuu wa taasisi kutoa michango yao NIC kadri watakavyotaka kuchangia kwa vipengele vitatu kisha pale watakapopata janga la kifo wataweza kupewa fedha zao kupitia wao au hata wategemezi wao.

“Tumekuwa tukipata misiba ya kuondokewa na wenza , watoto au wazazi wetu,  hivyo tumekuwa tukichangishana wenyewe kwa wenyewe, nikaona hii bidhaa itasaidia sana kunusuru kila mmoja kuingia mfukoni kuchangia, na badala yake Bima ifanye kazi hiyo” amesema Mkeyenge.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here