Na; Hughes Dugilo, DODOMA
Shirika la Bima la Taifa (NIC) limetoa elimu ya masuala ya Bima kwa wananchi waliotembelea maonesho ya kilimo ya kimataifa (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya nzuguni Jijini Dodoma.
Akizungumza katika maonesho hayo, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Shirika hill Karimu Meshack amesema kuwa lengo LA kutoa elimu hiyo ni kuwawezesha wananchi kutatua changamoto zinazowakabili wakulima kwakushindwa kukata Bima mazao yao kutokana na kukosa uelewa na elimu sahihi ya Bima hiyo.
Ameeleza kuwa NIC imefanya utafiti na kutambua kuwa wakulima wanapatwa na majanga mbalimbali ikiwemo viashiria na changamoto ikiwemo mvua kupita kiasi na ukame zinaharibu mazao yao.
“Sisi kama Shirika tumeweza kutambua changamoto za wakulima ambazo zinawathiri ikiwemo wanyama wakali ambao wanavamia mazao shambani, pamoja na mvua nyingi zinazozidi uwezo wa mimea kustahimili, na masuala ya ukame” amesema Meshack.
Aidha ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo wanatoa elimu kwa watanzania wote nchini hususani wakulima walioko Dodoma na mikoa ya jirani na hivyo kuwakaribisha kutembelea Banda lao ili kupata elimu.
“Tuna wataalamu ambao wanatoa elimu bora ya Bima yenye lengo la kumuweza mkulima kupata fidia pindi anapopatwa na majanga kwani tunaweza kurejesha fedha hiyo ili uweze kurudi shambani” ameongeza.