Home BUSINESS NELSON MANDELA YAPONGEZWA KWA KUUNGANISHA JAMII KUPITIA BUNIFU

NELSON MANDELA YAPONGEZWA KWA KUUNGANISHA JAMII KUPITIA BUNIFU

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe.Remidius Mwema (Kulia) akipata maelezo kuhusu bunifu ya Funza Lishe inayozalishwa na taka ya mkonge kwa ajili ya chakula cha Mifugo na Mbolea kutoka kwa Mbunifu Aziza Konyo (Kushoto) leo Agosti 4, 2024 alipotembelea banda la Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela katika Maonesho ya Nanenane viwanja vya Themi Njiro Jijini Arusha.

…….

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Emanuel Mwema ameipongeza Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kwa kuitendea kazi kauli mbiu ya Taaluma kwa Jamii na Viwanda kupitia bunifu za funza lishe na mtambo wa kisasa wa kuchakata taka na kuzalisha mbolea asilia hivyo kuwawezesha Wakulima na Wafugaji kupata mazao bora.

Mhe. Remidius ameyasema hayo Agosti 4, 2024 alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya 30 ya Kilimo na Mifugo na Sherehe za Wakulima Nanenane 2024 Kanda ya Kaskazini viwanja vya Themi Njiro Jijini Arusha.

“Hii inadhihirisha wazi kuwa kuna watanzania wenye uwezo wa kukaa na kufikiria kwamba kuna changamoto fulani na baadaye kuja na suluhisho kupitia utafiyi na bunifu mbalimbali kama nilivyoziona hapa” anasema Mkuu wa Wilaya Mhe. Remidius.

Ameongeza kwa kueleza kuwa, Serikali imeweka mkaza kwenye ustawi wa kilimo hivyo kupitia bunifu za mbolea asilia na funza lishe zitasaidia katika kupata matokeo bora ya mazao ya kilimo na mifugo.

Aidha Mkuu wa Wilaya Mhe. Remidius ametoa wito kwa Taasisi hiyo kutembelea wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara ili kutoa Kuhamasisha wanafunzi na wananchi umuhimu wa Sayansi na Teknolojia ili kuendana na kasi ya maendeleo ya Teknolojia.

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela inashiriki katika maonesho ya Nanenane kwa kuonyesha tafiti na bunifu za Uji Tayari, Funza Lishe, Mtambo wa Kisasa wa Kuchakata Taka na Kuzalisha Mbolea Asilia, Mtambo wa Kuchuja Maji wa NanoFilter , Chanjo ya Samaki , huduma ya kupima afya ya akili na vikundi vya kijamii vya wajasilimia mali.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe.Remidius Mwema (Kulia) akipata maelezo kuhusu bunifu ya Funza Lishe inayozalishwa na taka ya mkonge kwa ajili ya chakula cha Mifugo na Mbolea kutoka kwa Mbunifu Aziza Konyo (Kushoto) leo Agosti 4, 2024 alipotembelea banda la Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela katika Maonesho ya Nanenane viwanja vya Themi Njiro Jijini Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe.Remidius Mwema (Katikati mwenye kofia) akipata maelezo kuhusu bunifu ya Mtambo wa kisasa wa kuchakata na kuzalisha mbolea asilia kutoka kwa Mbunifu Petro Mwamlima (Kulia) leo Agosti 4, 2024 alipotembelea banda la Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela katika Maonesho ya Nanenane viwanja vya Themi Njiro Jijini Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe.Remidius Mwema (Kulia) akipata maelezo kuhusu bidhaa ya Uji Tayari kutoka kwa Bi. Rufina Fredrick (Kushoto) leo Agosti 4, 2024 alipotembelea banda la Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela katika Maonesho ya Nanenane viwanja vya Themi Njiro Jijini Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe.Remidius Mwema (Kulia) akipata maelezo kuhusu kifaa cha kutathmini utendaji kazi wa ubongo, kupitia mradi wa CEREBRAM (Center for Research of Brain and Mind) ikiwa ni utafiti unaofanywa na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kwa kushirikiana na Sapien Labs ya nchini Marekani alipotembelea banda la Taasisi hiyo Agosti katika Maonesho ya Nanenane viwanja vya Themi Njiro Jijini Arusha.

Previous articleUDOM WAJA NA UTAFITI WA TIBALISHE KUPUNGUZA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA
Next articleMAKAMU WA RAIS ASHIRIKI KILELE CHA WIKI YA MWANANCHI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here