Home BUSINESS MCHECHU: RC MAKONDA NI KIONGOZI MBUNIFU

MCHECHU: RC MAKONDA NI KIONGOZI MBUNIFU

ARUSHA 

Msajili wa Hazina nchini Tanzania Bw. Nehemia Mchechu amewataka wakuu wa mikoa mingine kuchukua ubunifu na uchapakazi wa Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha kama changamoto kwao ya kuhakikisha wanatumia vyema fursa mbalimbali kwenye mikoa yao.

Mchechu amebainisha hayo mapema jioni ya leo Agosti 29, 2024, wakati wa hafla maalum, iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuwashirikisha wakuu wa Taasisi, mashirika na wakala za serikali pamoja na wafanyabiashara kutoka Mkoani hapa kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kupeana fursa mbalimbali.

“Makonda anachokifanya na watu wa Arusha ni changamoto kwa wakuu wa mikoa wa sehemu nyingine kuwa Mgeni akija, wewe mwenye nyumba faidika kwa kuhakikisha kwamba unayakamilisha yako kwa urahisi zaidi palepale. Mikutano hii inapofanyika maeneo mengine waangalie ujanja na ukarimu wa kuwaita”, Amesema Mchechu.

Katika hatua nyingine Dkt.Maulid Maulid, Mtendaji mkuu wa Taasisi ya maendeleo ya waalimu amemtaja Mhe. Paul Makonda kama kiongozi wa mfano kutokana na namna anavyojishughulisha na masuala ya wananchi wake na kuhakikisha anawaunganisha na fursa mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here