Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam ( DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika leo Agosti 7, 2024 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano Cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Afisa Uhusiano Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika leo Agosti 7, 2024 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano Cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Afrika Mashariki Deodatus Balile akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika leo Agosti 7, 2024 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Bi. Everlasting Lyaro akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kilichofanyika leo Agosti 7, 2024 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kaika kikao kazi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam ( DAWASA) kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imefanikiwa kufikisha huduma ya maji kwa asilimia 93 katika Mikoa yote ya 23 ya kihuduma huku wakitegemea Mto Ruvu kuwa chanzo kikuu cha maji ambacho kinachangia asilimia 87 katika uzalishaji wa maji.
Hayo yameelezwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire, katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika leo Agosti 7,2024 Jijini Dar es Salaam, chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Katika wasilisho lake, Mhandisi Bwire. ameelezea Dawasa inavyotekeleza majukumu yake huku ataja vyanzo mbalimbali vya maji wanavyo vitegemea kufikisha huduma ya maji wanavyotegemea ni Mto Kizinga ambao unachangia asilimia mbili pamoja na Visima vya maji vilivyopo Kigamboni Kimbiji.
Mhandisi Mkama Bwire amesema kuwa bado wanaendelea kufanya jitihada ili kuhakikisha mtandao wa kiliomita 7, 087 unaotoa huduma unakuwa na ufanisi mkubwa na kuleta matokeo chanya kwa wananchi.
“Tumefikisha huduma ya maji kwa asilimia 93 katika maeneo yote ya DAWASA, changamoto iliyopo baadhi ya maeneo bado hatujasambaza mtandao wa maji, lakini tunaendelea na utekelezaji ili wananchi waweze kupata huduma” amesema Mhandisi Bwire.
Amesema kuwa wanaendelea kuboresha maeneo ya kutoa huduma ya maji takribani mikoa ya kihuduma 23, lakini ilani inawataka ifikapo mwaka 2025 wawe wamefikisha asilimia 95 ya kutoa huduma ya maji kwa wananchi.
Ameeleza kuwa kwa sasa maeneo mengi yanapata huduma ya maji muda wote, lakini maeneo mengine wapo katika hatua ya kufikisha huduma ya maji kwa kusambaza mtandao wa mapomba na kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma ya maji safi na salama.
“Ukienda maeneo ya kigamboni kuna maji ya kutosha, kinachotakiwa kwa sasa kuongeza kasi ya uzambazaji wa mtandao wa mabomba katika maeneo yote yenye changamoto” amesema Mhandisi Bwire.
Mhandisi Bwire amesema kuwa kuna jumla ya matanki 138 yenye uwezo wa kuifadhi maji lita 183,649,000 na kuweza kutoa huduma kwa masaa yasiyopungua sita.
Amesema kuwa kutokana na uhitaji bado wanaitaji nguvu kutoka sekta binafsi ya kuongeza vyanzo vya maji, huku akieleza kuwa hivi karibuni wanatarajia kupata vyanzo vingine kutoka Mto Rufiji, pamoja na Bwawa la Kidunda.
Mhandisi Bwire amesema kuwa ujenzi wa Bwawa la Kidunda utaboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa wananchi kwa kuhakikisha yanapatikana muda wote katika Mikoa ya Dar es Salaam pamoja na Pwani.
Amesema kuwa ujenzi wa Bwawa Kidunda unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya sita unatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 300 ambao unatekelezwa na Mkandarasi kutoka kampuni ya Sino Hydro Corporation kutoka nchini China.
“Kukamilika kwa mradi wa kidunda utawezesha mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini kuzalisha jumla ya lita milioni 466 kwa siku na kuzalisha maji muda wote na kuondoa changamoto ya ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo” amesema Mhandisi Bwire.
Mhandisi Bwire amesema kuwa licha ya kutoa huduma katika Mkoa wa Dar es Salaam, pia wanatoa huduma ya maji baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Tanga, Morogoro pamoja na Pwani